Diamond Platnumz kushikiliwa na polisi baada ya Kumkana mtoto wake mwingine.

Msanii Diamond Platnumz ameingia tena matatani baada ya mwanamke mmoja kutokea nchini kenya kudai kuwa amezaa na staa huyo. Inadaiwa kuwa mwanamke huyo aliwasili nchini Tanzania Mapema Mwezi uliopita na kuanza jitihada za kumtafuta msanii huyo ili ampe pesa za matumizi za mwanae huyo, Baada ya kumkosa aliamua kuweka makazi njee ya nyumba ya Msanii Huyo kwa mda wa takribani siku tano bila mafanikio yoyote,

 

Baada ya kutokufanikiwa kumpata msanii huyo mama huyo aliamua kuripoti katika kituo cha polisi kwa ajili ya kutafuta uwezekano wa kumpata msanii huyo kwa nguvu ya serikali. Alidai kuwa hii sio mara yake ya kwanza kuweza kuwasili Nchini Tanzania kwani hata katikati ya mwaka huu aliweza kuja nchini Tanzania kumtafuta mwanamziki huyo lakini jitihada zake ziligonga mwamba.

Kwa sasa polisi wanaendelea kufuatilia kesi hiyo na kutafuta uwezekano wa kuongea na msanii huyo ili waweze kuyamaliza maswala hayo.

 

IMG_20171230_172436[1]

 

Advertisements

Leave a Reply

Please log in using one of these methods to post your comment:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s