Basata wakataza Wasafi festival kufanyika kenya.

Wakati msanii Diamond Platnumz na mwenzake Rayvanny wakiendelea kutumikia adhabu ya kufungiwa kufanya tamasha lolote nchini na kufungiwa kwa Wasafi festival nchini tanzania huku chanzo cha kufungiwa kikiwa ni baada ya kuimba wimbo unaojulikana kwa jina la Mwanza ambao ulifungiwa na Baraza la sanaa Basata wiki kadhaa zilizopita walipokuwa wakifanya Tamasha la Wasafi festival huko jijini Mwanza.

Hatimaye Baraza Hilo la Sanaa Tanzania limejitokeza na kudai ya kwamba halijampa kibali msanii huyo Diamond Platnumz kufanya tamasha hilo nchini kenya kwana Baraza hilo la sanaa lilitoa tamko la kufungia Tamasha hilo kutokufanyika kwa mda usiojulikana.

Katibu mkuu wa Basata Godfrey Ngereza amedai ya kwamba Baraza hilo la sanaa Tanzania halijatoa kibali kwa msanii huyo Diamond Platnumz kufanya Tamasha hilo huko nchini kenya na Kumuomba msanii huyo atii masharti na kanuni za Baraza hilo la sanaa Tanzania.

Ikumbukwe kuwa siku ya jana msanii huyo Diamond Platnumz alidai ya kwamba Tamasha la wasafi festival limefungiwa tu nchini Tanzania na kwa upande wa Kenya Tamasha hilo litaendelea kama kawaida.

46712225_2229998247324261_7516128136780411829_n.jpg

Advertisements

Leave a Reply

Please log in using one of these methods to post your comment:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s