Uraia wa watu waliokuwemo kwenye ndege iliyopata ajali watambuliwa

Addis Ababa Ethiopia, Shirika la ndege la Ethiopia limetaja Raia na Mataifa ya watu waliopata ajali, kwenye ndege ya shirika hilo iliotokea jana asubuhi.

Kwa mujibu wa taarifa ya Shirika la Ndege la Ethiopia, ndege hiyo iliruka saa 2:38 asubuhi kwa saa za Ethiopia kutokea uwanja wa ndege wa kimataifa wa Bole na kwamba watu waliokuwemo ndani ya ndege hiyo wanatoka katika nchi 33.

“Kwa wakati huu, oparation ya utafutaji na uokoaji wa miili unaendelea na hatuna taarifa zilizothibitishwa za waliopona au waliojeruhiwa kwenye ajali hii. Wafanyakazi wa shirika hili wamekwenda eneo la tukio na watafanya jitihada zozote kutoa huduma za dharula” Taarifa iliyotolewa na shirika hilo.

Msemaji wa shirika hilo Asrat Begashaw alinukuliwa na Shirika la habari la kitaifa la Ethiopia akisema kuwa hakuna hata mmoja alienusurika katika Ajali hiyo, Wote wamekufa.
Kampuni hiyo imesema imeanzisha kituo cha kupata taarifa kuhusu familia na marafiki za watu waliokuwemo ndani ya ndege hiyo.

Advertisements

Leave a Reply

Please log in using one of these methods to post your comment:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s